![]() |
| Wachimbaji wa dhahabu nyeupe Afrika kusini |
MAELFU ya
wafanyakazi wa migodi ya dhahabu nyeupe nchini Afrika kusini wamerudi kazini
kufuatia makubaliano ya malipo yao ya miaka mitatu ya kumaliza mgomo ambao
umedumu kwa muda wa miezi mitano.
Baada ya kutokuwa kazini kwa muda
mrefu wafanyakazi hao watapewa mafunzo na kufanyiwa ukagauzi wa kiafya nahuenda
ikachukua miezi kadha kabla ya shughhuli kwenye migodi kurejelea hali ya
kawaida.
Mgomo huo unakisiwa kugharimu
makampuni hasara ya dola bilioni mbili na kusababasha kudorora kwa uchumi wa
afrika kusini.
Chama cha wafanyakazi hao cha AMCU
kilitia sahihi mapatano mbalimbali na kampuni za Lonmin, Impala na Anglo
American hiyo yana.
Wafanyakazi hao hawakupata mshahara
waliotarajia wa Rand za Afrika Kusini 12,500 (zaidi ya Dola 1,000) lakini
walikubali mkataba wa miaka mitatu ambapo wataendelea kuongezwa mshahara,
penisheni, malipo ya nyumba na bima ya Afya.
Tayari wafanyakazi hao wamerudi
kazini katika machimbo hayo ya dhahabu nyeupe hii leo lakini ni dhahiri kuwa
itachukua miezi kadhaa kabla ya uzalishaji wa madini hayo kufikia hali yake ya
kawaida.
Mkataba huo wa miaka mitatu uliotiwa
sahihi pamoja na kampuni za Lonmin, Impala Platinum na American Platinum
imemaliza mgomo mrefu zaidi kuwahi kutokea nchini Afrika Kusini na ambao
umegharimu taifa pesa nyingi sana.
Wazalishaji wa dhahabu nyeupe
walipata hasara ya Dola Bilioni 2 na wafanyakazi hao wakapoteza mishahara ya
Dola Bilioni moja tangu mgomo huo uanze Januari mwaka huu.

No comments:
Post a Comment