![]() |
| Bi Merian Ibrahim akiwa na Mumewe |
MWANASHERIA wa mwanamke wa Sudan aliyekamatwa siku chache baada ya kuhukumiwa kifo kwa kuasi dini ya Kiislam kwa kuolewa na
Mkristo, amesema mteja wake anatuhumiwa kwa kughushi nyaraka za safari.
Amesema mwanamke huyo Meriam Ibrahim
bado anashikiliwa katika kituo cha polisi katika mji Mkuu wa Khartoum.Sudan
Kusini ambayo ndio iliyompa nyaraka hizo imesema kuwa nyaraka hizo ni halali
kwa vile ameolewa na mwanaume raia halisi wa Sudan Kusini.
Mwanasheria wa Meriam Ibrahim
amesema yeye pamoja na mumewe walikuwa wakiohojiwa kuhusuana na hati za
kusafiria. Ilikuwa inasadikiwa kuwa walikuwa wanasafiri kuelekea nchini
Marekani.
Awali Marekani ilisema itashirikana
na Sudan kuhakikisha kuwa mwanamke aliyesamehewa hukumu ya kifo kwa kuasi dini
ya Kiislam anaruhusiwa kuondoka nchini humo baada ya kukamatwa katika uwanja wa
ndege wa Khartoum.
Mwanamke huyo Meriam Ibrahim,
alihukumiwa kifo kwa kosa la kuolewa na mwanamume mkristo na kukana dini ya
kiisilamu alikamatwa akiwa na familia yake katika uwanja wa ndege mjini
Khartoum.

No comments:
Post a Comment