![]() |
| Mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Amanzi akiongea na waandishi wa habari |
UTAFITI wa
ukatili na unyanyasaji kwa wanawake na watoto uliofanywa hivi karibuni na Taasisi
ya Tanzania Women Health Network TWHN Manispaa ya Morogoro umebaini zaidi ya
asilimia 62 ya watoto katika manispaa hiyo wamefanyiwa ukatili
Kisaikolojia,Jinsia na kimwili na watu wa karibu wakiwemo ndugu na jamaa.
Hayo yamo kwenye taarifa fupi ya uzinduzi wa Taasisi hiyo
iliyosomwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo nchini Gloria Kasilo kwa Mkuu wa
wilaya ya Morogoro Said Amanzi aliyewakilishwa na Afisa elimu Taaluma Manispaa
hiyo Christopher Wangwe.
Mbali na utafiti huo Mkurugenzi Gloria alisema Taasisi hiyo
inayopambana na ukatili kwa mama na mtoto unakua kila siku ambapo takwimu za
kimataifa za 2011 zinaonyesha kati ya watoto 10 wa kike sita wamefanyiwa
ukatili huo majumbani,shuleni na mitaani ambapo kupitia taasisi hiyo kati ya
10,saba wamefanyiwa uakatili.
Alisema lengo la Taasisi hiyo ni kumwezesha mwanamke hasa mtoto wa
kike kujikomboa kwa kupata elimu itakayomwezesha kuzikabili changamoto
zinazowakabili katika mazingira walipo,aweze kujisimamia na kumtoa kwenye
utegemezi na kujiletea maendeleo.

No comments:
Post a Comment