![]() |
| Afisa wa Mamlaka ya chakula na dawa nchini( TFDA) akiongea na wanahabari |
MAMLAKA ya chakula na
dawa nchini (TFDA) imeitaka jamii ya watanzania kuwafichua watu wanaofanya
biashara ya vipodozi visivyoruhusiwa na serikali kwa kuwaripoti nkatika ofisi
za mamlaka hiyo.
Wakiongea na Mbiu ya Maendeleo katika viwanja vya Mnazi
mmoja jijini Dar es salaama katika
maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa umma yanayoendelea katika viwanja hivyo watumishi mamlaka hiyo wamesema kuwa mapambano
dhidi ya vipodozi haramu yatafanikiwa endapo wananchi watashiriki kikamilifua
katika kuwafichua wafanyabiashara wanaokiuka taratibu za uagizaji na uingizaji
wa vipodozi vuisivyoruhusiwa.
Wamesema,
kwa mujibu wa tafiti walizozifanyaimebainika kuwa wafanyabiashara wa vipodozi vilivyopigwa
marufuku ni watu wenye historia ya kufanya makosa makubwa ya uhalifu hivyo ni
vyema mapambano hayo yakashirikikisha kila mdau .
Mbali na Vipodozi Mamlaka hiyo inashughulikia
uuzaji wa bidha zilizokosa viwango na kuisha muda wake.

No comments:
Post a Comment