Sunday, June 22, 2014

MAADHIMISHO ya wiki ya Utumishi kufungwa kesho



Katibu mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
MAADHIMISHO ya wiki ya Utumishi wa umma yanatarajiwa kugfungwa kesho jioni baada ya takribani wiki moja ya kuonesha wananchi shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi mbalimbali za wizara hapa nchini.


Akiongea na Mbiu ya Maendeleo mapema leo katika viwanja vya Mnazi mmoja ,jijini Dar es salaam,Muwezeshaji toka wizara ya maliasili na Utalii amesema kuwa , wananchi wamejifunza mengi toka katika banda la wizara hiyo yenye jukumu la kutunza maliasili za
Taifa ikiwa nipamoja na kupata maelezo ya namana ya kupambana na ujangili wa maliasili hasa meno ya Tembo.

Amesema, kwa wananchi wanaohitaji kupata mengi kuhusu majukumu na kazi mbalimbali za wizara hiyo wanakaribishwa kwenye maonesho ya sabasaba yanayotarajiwa kuanza tarehe 28,juni 2014 siku ya jumamosi na kumalizika tarehe08,kwa kuwa wanatarajia kushirikia kwenye maonesho hayo.
 
Mgeni rasmi wa kufunga wiki ya madhimisho ya wiki ya Utumishi wa umma anatarajiwa  kuwa Katibu mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.

No comments:

Post a Comment