Sunday, June 22, 2014

WAZIRI wa mambo ya nje wa Marekani azuru nchini Misri


 
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry
WAZIRIwa mambo ya nje  nchini Marekani John Kerry amewasili  nchini Misri kwa lengo las kukutana na rais mpya wa Misri Abdul Fatah Al Sisi.
Waziri huyo wa Marekani  ndiye kiongozi wa kwanza kutembele nchi ya  Misri tangu kamanda huyo wa zamani wa jeshi kuchaguliwa kama rais baada ya kumpindua aliyekuwa rais wa Taifa hilo Mohammed Morsi.


Maafisa wa Marekani wanasema kuwa lengo kuu la bwana Kerry kuzuru nchi hiyo ni kumtaka rais Abdul fatah Al sisi kuwashirikisha watu wote katika siasa yake ikiwemo wanachama wa kundi la Muslim Brotherhhood lililopigwa marufuku.

Kerry pia anatarajiwa kuzungumzia kuhusu hukumu ya kifo iliotolewa dhidi ya wanachama wengi wa kundi hilo mbali na kutoa wito wa kuachiliwa kwa waandishi waliofungwa.

Kwa mujibu wa vyombo vvya habari vilivyoongozana na kiongozi huyo wa Marekani vinasema kuwa,  bwana kerry amesema kuwa Marekani iko tayari kuanzisha mazungumzo na rais huyo mpya ikiwa na matumaini kwamba mazungumzo hayo yataleta natija.

No comments:

Post a Comment