Saturday, June 21, 2014

WAKILI asema mahakama imezingatia sheria hukumu ya kifo cha wanachama 182 wa kundi la Ikwaan Muslim


Wanachama wa Muslim Brotherhood wakiwa mahakamani

WAKILI  mmoja nchini Misri ameiambia ameviambia vyombo vya habari  kwamba mahakama imezingatia hukumu ya kifo cha wanachama 182 wa kundi la Muslim Brotherhood .

Washitakiwa hao ni miongoni mwa watu 700 wanaoshtakiwa kwa kukishambulia kituo kimoja cha polisi katika eneo la Minya mwaka uliopita.
Miongoni mwa watu waliohukumiwa  kifo ni pamoja na kiongozi wa kundi hilo Bwana Mohammed Badie .
Washtakiwa wengine watano walipewa hukumu nyingine ya kati ya miaka 15 na 55 huku wengine wakiachiliwa huru.
Hukumu iliotolewa mnamo mwezi Aprili ambapo jaji aliwapatia hukumu ya kifo washitakiwa wote ilizua pingamizi kutoka kwa makundi ya kupigania haki za kibinaadamu.

No comments:

Post a Comment