AFISA mwandamizi wa shirika la madaktari wasio na Mipaka Medicine San
Frontiers ameelezea kuwa mripuko wa ugonjwa wa Ebola katika mataifa matatu ya
magharibi hauwezi kudhibitika.
Mkurugenzi wa Oparesheni
katika shirika hilo Bart Janssens ameliambia shirika la habari la A.P kwamba
ugonjwa huo utasambaa hadi katika mataifa mengine iwapo hakutakuwa na mwitikio
wa kimataifa.
Ugonjwa wa Ebola
tayari umesababisha vifo vya takriban watu 330 nchini Guinea,Sierra leone na
Liberia.
Bwana Janssens
amesema kuwa shirika la MSF limefikia kikomo cha uwezo wake wa kukabiliana na
ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment