Wanajeshi nchini Yemen |
YEMEN imesema wapiganaji wa
kundi la al-Qaeda wamewaua watu sita katika mapigano na vikosi vya serikali
kaskazini mwa jimbo la Abyan.
Mwezi April, serikali ya nchi hiyo ilizindua operesheni maalumu ya kuwaondoa wapiganaji wa kundi hilo katika jimbo la Abyan na maeneo jirani ya jimbo la Shabwa.
Hata hivyo ripoti za mapema leo hii zinasema watu kadhaa wameuawa katika mapigano kati ya maejshi ya serikali na wapiganaji wa kundi la Shia wanaojulikana kama Houthis.
Vikosi vya anga vya Yemeni vimekuwa vikishambulia ngome za Al Sahabab ndani na nje ya mji wa Amran kuanzia jana.
No comments:
Post a Comment