Sunday, July 6, 2014

UMOJA wa maulamaa nchini Iraq walaani vitendo vya kubomolewa misikiti


Masheikh wa Kisuni nchini Iraq

UMOJA  wa maulama wa Kiislamu wa madhehebu ya Kisuni nchini Iraq umelaani vitendo  vya kubomolewa misikiti ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni na Shia vinavyofanywa na magaidi wa kitakfiri wa kundi linalojiita eti Dola la Kiislamu la Iraq na Sham (Daesh) katika mkoa wa Nainawa nchini humo.

Mbali na kulaani vitendo hivyo, umoja huo umeitaja jinai hiyo kuwa inayokinzana na misingi ya dini ya Kiislamu na umetaka kukomeshwa mwenendo huo mara moja.
Wakati huo huo zaidi ya wapiganaji wa genge hilo la kitakfiri wapatao 100 akiwemo kiongozi wa kundi hilo anayeitwa Husein Farras al-Mash’hadan maarufu kwa jina la Abu Hammam na walinzi wake, wameuawa na askari wa Iraq kaskazini mwa mji mkuu Baghdad.
Msemaji wa ofisi ya kamanda mkuu wa majeshi ya Iraq Fariq Qasim Atwa amewambia waandishi wa habari leo kwamba magaidi 20 yameuawa katika mripuko uliotokea karibu na jengo la bunge la mkoa wa Salahudin, huku wengine 90 waliokuwa wakijaribu kushambulia eneo la Beiji nchini humo wakiuawa na jeshi la taifa.


No comments:

Post a Comment