TAARIFA kutoka nchini Israeli zinasema kuwa serikali inawazuia
baadhi ya watu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kijana wa kipalestina
Mohammed Abu Khdeir.
Mauaji hayo kwa mujibu wa polisi
nchini humo yanahusishwa na hamasa za utofauti wa utaifa .
Hata hivyo mauaji hayo yamechukuliwa
kama ni ulipizaji kisasi dhidi ya mauajia ya wanaharakati wa kiyahudi kutokana
na kuuawa kwa vijana watatu mwezi uliopita.
Israel imeyatuhumu makundi ya
kijeshi ya wapiganaji wa Kipalestina wa Hamas kwa mauaji hayo.
Kundi la Hamas wao wamekanusha
kuhusishwa na mauaji hayo.
Idara za usalama za Israeli
zinamshikilia raia wa Palestina anayedaiwa kuhamasihsa mauaji hayo ya vijana wa
Israel.
No comments:
Post a Comment