Shamba la mtama kijiji cha Mihugwe, Kisarawe pwani |
WANANCHI wa kijiji cha Mihugwe tarafa ya Mzenga, wilayani
Kisarawe mkoa wa PWANI wamehimizwa
kulima zao la mtama ili kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya
nchi inayoikabili wilaya hiyo kwa kasi sana.
Akiongea na Mbiu ya Maendeleo katika
kijiji hicho Mwenyekiti wa kijiji cha Mihugwe Bwana Zoyo amesema kuwa, zao la
mtama limewaokoa kwa mwaka huu kutopkana ana na mazao mengine kushindwa
kuastahili ukame , hivyo wanankijiji wengi wana uhakika wa chakula .
Hata hivyo mwenyekiti huyo ameiomba
serikali na wadau wa maendeleo kuwawezesha ujuzi wa namna kuzalisha zao la mtama kibiashara si kujitosheleza kwa chakula pekee.
No comments:
Post a Comment