Ujenzi wa Bwawa la Annahdha |
MISRI imetangaza kuwa
Ethiopia imeafiki kushiriki katika kikao cha pande tatu kitakachoshirikisha
wawakilishi wa nchi hizo mbili na Sudan kujadili ujenzi wa bwawa la Annahdha
juu ya maji ya Mto Nile.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Vyanzo vya Maji ya Misri
imesema kikao hicho kimepangwa kufanyika wiki ya tatu ya mwei ujao wa Agosti
mjini Khartoum, Sudan.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa Ethiopia imekubali wito wa
Misri wa kushiriki katika kikao cha pande hizo tatu kitakachojadili athari za
ujenzi wa bwawa wa Annahdha katika maji ya Mto Nile.
Kikao hicho kitakachohudhuriwa na Mawaziri wa Maji wa nchi
hizo tatu kitajadili pia fungu la maji ya Misri na Sudan katika maji ya Mto
Nile.
Serikali ya Misri inapinga ujenzi wa bwawa la Annahdha katika Mto Nile na kutokana na ukweli kwamba asilimia 85 ya maji ya Misri yanatokana na maji ya mto huo. Baadhi ya wanasiasa wa Misri pia waliwahi kutoa pendekezo kuihujumu Ethiopia au kuyasaidia makundi ya waasi dhidi ya serikali ya Addis Ababa iwapo haitatupilia mbali mradi wake wa ujenzi wa bwawa hilo katika Mto Nile.

No comments:
Post a Comment