Thursday, July 17, 2014

WAISLAMU duniani wakumbushwa kukithirisha ibada katika kumi la mwisho

Masjid jamia,Nairobi nchini Kenya

WAISLAMU  katika baadhi ya maeneo ya dunia usiku wa kuamkia leo wamehuisha usiku wa kwanza kati ya usiku zinazotarajiwa kuwa ni usiku wa Lailatul Qadr ambao umetajwa katika kitabu kitakatifu cha Qur'ani kuwa ni bora kuliko miezi elfu moja.
Katika usiku huo unaosadifiana na mkesha wa tarehe 19 Ramadhani Waislamu hukesha misikitini na maeneo ya ibada katika hali ya kuomba dua, kuswali na kumtaradhia Mola Muumba.

Nchini Iran jana usiku mamilioni ya waumini walikesha katika misikiti na maeneo mengine ya ibada wakihuisha usiku huo kwa dua, maombi, swala, kiraa ya Qur'ani na kunong'ona na Mola Karima.

No comments:

Post a Comment