Shannon Richardson akiwa mahakamani |
MUIGIZAJI mwanamke nchini Marekani aliyemtumia
Rais Barack Obama barua iliyokuwa na sumu ya Ricin amefungwa jela kwa miaka 18.
Shannon Richardson,
mwenye umri wa miaka 36, kutoka Texas, pia alimtumia meya wa New York Michael
Bloomburg barua nyingine iliyokuwa na sumu hiyo hiyo.
Alidai kuwa mumewe
waliyeachana naye ndiye alituma barua hizo katika njama ya kumlimbikizia madai
hayo.
"sikuwa na nia ya
kumdhuru mtu, '' Shannon aliambia mahakama.
Alikiri kosa la
kumiliki na kutengeza sumu hiyo mwezi Disemba.
Jaji alimpa hukumu
kubwa zaidi ikilinganishwa na kosa lake na pia kutakiwa kulipa faini ya dola
367,000.
Richardson, mama
mwenye watoto six, ameigiza katika vipindi kama 'The Vampire Diaries' na 'The
Walking Dead.'
Viongozi wa mashitaka
wanasema kuwa mwanamke huyo aliagiza bidhaa za kutengeza sumu hiyo kupitia kwa
mtandao kisha akatuma barua tatu zilizokuwa zimepakwa sumu hiyo.
No comments:
Post a Comment