VUGUVUGU la kupigania Uhuru
wa Palestina, Hamas, na Israel
zimekubali kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza kwa muda wa saa tano
baadaye hivi leo baada ya siku tano za mapigano makali.
Baada ya ombi la umoja wa mataifa jeshi la Israel limesema kuwa litasitisha mashambulizi kati ya saa nne asubuhi hadi saa tisa kwa saa za Gaza, ili kuwaruhusu wakaazi kupata chakula na huduma muhimu.
Msemaji wa Hamas Sami Abu Zukhri amethibitisha kuwa vuguvugu hilo kadhalika litasitisha mashambulizi ya roketi dhidi ya Israel wakati huo.
Msemaji wa shirika la umoja wa mataifa linalowasaidia wakimbizi wa Palestina Christopher Gunnes amesema kuwa ni matumaini yake kwamba usitishaji huo wa mapigano utatoa fursa ya kusuluhisha matatizo yanayoikabili gaza.
No comments:
Post a Comment