Mkurugenzi mkuu wa PSPF Adamu Mayingu |
MFUKO wa hifadhi ya jamii PSPF umezindua mfuko wa mikopo maalumu
kwa wastaafu ukilenga kukomesha wimbi la umasikini na kuwawezesha kuishi maisha
bora hadi mwisho wa uhai wao.
Mbali na mfuko
huo kuanzisha mikopo kwa wastaafu na kufanikiwa kutekeleza mpango mkakati wa
‘PSPF tulizo la wastaafu’ uliowanufaisha zaidi ya wastaafu 2,000 tayari
umeanzisha huduma kwa simu za mikononi ijulikanayo ‘PSPF pamoja nawe’ na kituo
cha huduma kwa wateja Call
Center.
Hayo yalisemwa na
mkurugenzi mkuu wa mfuko huo Adam Mayingu kwenye mkutano wa 98 wa watayarishaji
wa vipindi vya elimu kwa umma kupitia shirika la utangazaji nchini TBC.
Katika maelezo
yake,Mayingu alisema mbali ya PSPF kufanikisha hayo pia imefanikiwa kutoa
huduma ya mafao sita kwa mfumo wa hiari sambamba na kuongeza idadi ya wanachama
kutoka 320,860 mwakajana hadi kufikia 400,000 kutoka katika sekta
mbalimbali nchini mwaka huu.
Akifungua mkutano
huo mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera ambae pia amejiunga na mfuko huo
aliutaka mfuko huo kujitangaza zaidi kutia vyombo vya habari ili wanachi
waufahamu na kuhamasika kujiunga.
Awali alilitaka shirika la
utangazaji nchini TBC kuendelea kutoa elimu zaidi ya uandaaji vipindi hivyo vya
elimu kwa umma na vinginevyo kuondoa changamoto ya habari holela.
Bendera alisema shirika hilo pia linapaswa kuwa
mstari wa mbele kuimarisha na kuboresha taaluma ya utangazaji kwa kuwajengea
uelewa waandaji wa vipindi kwa wamiliki na waongozaji katika
No comments:
Post a Comment