Aminu Sadiq Ogwuche |
MSHUKIWA wa
mashambulizi mawili ya mabomu mjini Abuja ,nchini Nigeria, ambayo yaliwaua watu
75 , amerejeshwa nchini Nigeria kutoka Sudan.
Aminu Sadiq Ogwuche, alikamatwa
mjini Khartoum mwezi Mei baada ya shirika la polisi wa kimataifa Interpol kutoa
waranti ya kumkamata.
Anatuhumiwa kwa kupanga mashambulizi
yaliyofanyika katika kituo cha basi mapema mwaka huu ambayo Boko Haram ilikiri
kuyafanya.
Maelfu ya watu wameuawa nchini
Nigeria mwaka huu peke kutokana na mashambulizi ya Boko Haram wakitaka
kuruhusiwa kuunda jimbo lenye kufuata sheria za kiisilamu Kaskazini mwa nchi.
No comments:
Post a Comment