Viongozi wa nchi wanachama wa BRICS |
.
Wakuu wa kundi hilo linaloundwa na Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini wametoa taarifa mwishoni mwa kikao chao Jumanne hii huko katika mji wa Fortaleza Brazil na kubainisha wasiwasi wao kuhusu taathira mbaya zinazosababishwa na ukosefu wa amani huko Iraq ikiwa ni natija ya kuongezeka vitendo vya makundi ya kigaidi nchini humo na kuyataka makundi yote ya Iraq kudumisha umoja ili kupambana na vitisho vya ugaidi.
Kundi la Brics pia limezitolea mwito pande za kieneo na kimataifa kuacha kuingilia na kuchochea mgogoro wa Iraq.
Nchi wanachama wa Brics pia zimeunga mkono juhudi za serikali na wananchi wa Iraq za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa sasa ili kuleta uthabiti na mshikamano nchini humo.
Katika upande mwingine nchi wanachama wa kundi la Brics zimetangaza kuwa kustafidi na nishati ya nyuklia ni haki ya wazi ya Iran na kusisitiza juu ya kupatiwa ufumbuzi kadhia ya nyuklia ya Iran kupitia njia za kidiplomasia na kisiasa.
No comments:
Post a Comment