Thursday, October 23, 2014

TUNDU Lisu aichambua katiba pendekezwa


Tundu Lisu

MWANASHERIA wa chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lisu ameichambua  kama Karanga katiba pendekezwa iliyoungwa mkono na Rais Jakaya Kikwete akisema ni ya kihistoria na bora kuliko zote ulimwenguni wakati akiipokea uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma.



Katika hotuba hiyo iliyowaacha mdomo wazi umati wa watu uliokuwa umefurika kumsiliza yeye na ujumbe wa kitaifa wakitokea jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya shule ya msingi Uwanja wa ndege mjini hapa alisema katiba hiyo ni chambo cha walala hoi kuikubali kwa faida ya walio nacho na madarakani.
Lisu alianza kuhutubia kwa kutaja baadhi ya maajabu na vioja vilivyotumika kupitisha katiba hiyo inayopingwa na umaja wa katiba ya wananchi UKAWA kuwa ni pamoja na ukiukwaji wa sheria za upigaji kura ikiwemo waliokufa,wagonjwa na waliokuwa kwenye ibada ikiwemo hija kupigishwa kura.

Alimtaja mama wa Zitto Kabwe, marehem Shida Salumu aliyefariki mwezi Julai na mwingine aliye msahau alisema wanahesabika kupigakura na kudhilisha kuwa lichokisema Kikwete mjini Dodoma wakati akikabidhiwa katiba hiyo ni ya kihistoria na bora kuliko katiba zote Ulimwenguni..
Kwa mujibu wa Lisu sababu za CCM kung’ang’ania katiba iliyopita ni kuendeleza ubwenyeye na ukabaila wa kumlibikizia rais madaraka ili walio madarakani na wenye nacho waendelee kujinehemesha kupitia rasilimali za nchi bila kuhojiwa kwamgongo na nembo ya Rais.

No comments:

Post a Comment