Abdulsalam Sas (katikati) na Mohamed Abdul azizi (kulia|) |
MBUNGE wa jimbo la Mikumi Abdulsalam
Ameri Sas amewataka wananchi jimboni humo kuacha kujipatia kipato kwa
njia haramu ikiwemo ya kujihusisha na ujangaili badala yake wajikite zaidi
katika ubunifu ikiwemo kuunda vikundi vya uzalishaji kama kuweka na kukopeshana
fedha.
Sas alisema hayo wakati akizindua tamasha la Ujirani Mwema la kupinga ujangili kwa wanyama waliohatarini kutoweka wakiwemo Tembo,Faru na Twiga lililoandaliwa na Mtandao wa habari za kijamii Tanzania ( MHAKITA).
Aliwataka wananchi hao kuunda vikundi vya ujasiliamali vitakavyowasaidia kujikwamua kiuchumi na sio kutegemea kuhujumu rasilimali za
nchi hasa mazo ya misitu.
No comments:
Post a Comment