![]() |
| Zainabu Al Khawaja |
MAHAKAMA moja ya nchini Bahrain imetoa amri ya kuwekwa kizuizi kwa siku saba mwanaharakati Zainab al Khawaja ili kusailiwa.
Hatua hiyo imejiri sambamba na kushadidi hatua za ukandamizaji za utawala wa al Khalifa dhidi ya wapinzani.
Wakili anayemtetea Zainab al Khawaja kwa jina la Mohammed al Wasti amesema kuwa amri hiyo imetolewa baada ya jaji wa mahakama hiyo ya Bahrain kumtuhumu mwanaharakati huyo kuwa alimfedhehesha Mfalme Hamad kwa kuchana picha yake wakati wa kusikilizwa kesi yake.
Zainab ambaye ni binti ya Abdulhadi al Khawaja mwanaharakati wa Bahrain aliyeko jela nchini humo, juzi alifikishwa mahakamani katika kikao cha kusikiliza kesi zake mbili za kukata rufaa za tangu mwaka 2012

No comments:
Post a Comment