![]() |
Waziri wa mambo ya ndani Mathias Chikawe |
WAZIRI wa
Mambo ya Ndani ya Nchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametahadharisha juu
ya kuongezeka kwa mitandao ya uhalifu wa kimataifa na ugaidi.
Kutokana na hali hiyo
waziri Chikawe amesema kuwa , kama haitadhibitiwa mapema na vyombo vya dola,
inaweza kujipenyeza katika sekta mbalimbali ikiwamo kufadhili watafuta uongozi
wa nchi.
Mathias Chikawe
amelitaka Jeshi la Polisi nchini Tanzania kupanga mikakati thabiti ya
kuhakikisha amani na utulivu uliopo nchini unaendelea kuimarishwa hasa wakati wa kampeni
na upigaji kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa. Amesema,.
Uhalifu wa
kimataifa hutumia fedha chafu zinazopatikana kwa njia haramu na kuwa ni hatari
kwa usalama wa taifa kutokana na kwamba kutokana na uwezo mkubwa wa kifedha wa
mitandao hiyo, ni rahisi kujipenyeza hata katika uongozi. Kuhusu kuibuka kwa
makundi ya kihalifu kama vile 'Panya road', Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa
Tanzania amesema, hali hiyo haikubaliki na kulitaka Jeshi hilo kutimiza wajibu
badala ya kusubiri matukio yatokee.
No comments:
Post a Comment