Tuesday, January 27, 2015

ULANGA waomba msaada wa uwezeshwaji toka FCS



Jengo la Halmashauri ya Ulanga, Morogoro

WANANCHI wilayani Ulanga,  waiomba Shirika la Foundation For Civil Society kuzipa kipaumbele AZAKI zenye lengo la kutoa elimu  ya uraia wilayani humo ili kufahamu haki na wajibu. 
 Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya mada ya Utawala bora kuwasilishwa na wanasheria Angelus Lunji katika mafunzo ya ufuatiliaji rasilimali za umma sekta ya Afya yaliyoandaliawa na asasi ya Kijogoo group na FCS mjini Mahenge,walisema wilaya hiyo iko nyuma kimaendeleo kwa kukosa elimu.

Yoleta na Laza Mwandwani walibainisha kuwa wilaya ya mahenge inashindwa kuendelea kutokana na wilaya hiyo kuwa kugeuzwa shmba la bibi katika sekta zote za kiutawala kwa kuwa wanachi wake wamejaa hofu na uoga wa kuhoji mabo mbalimbali ya kimaendeleo.

Walisema katika wilaya hiyo Elimu ni duni,hakuna maji,umeme,huduma za Afya ni janga huku miundombinu hasa vijijini ikibaki janga lisilo na jibu la ufumbuzi kama kilio cha Samaki majini machozi kwenda na maji.

Wakizungumzia suala la uduni wa huduma za Afya,baadhi yao kutoka kata ya Nawenge na Msogezi walikili kuzikosa huduma za afya jirani na vijiji walipo kutokana na wanachi kuhofu kuhoji kwenye mamlaka husika juu ya suala hilo.

Awali Mkurugenzi wa Asasi ya Kijogoo Ramadhan Omari na mtaalamu wa uwezeshaji katika ufuatiliaji rasilimali za umma mkoani Morogoro Rajabu Hussen waliwasihi kutotumia jaziba katika shuguli hiyo na kuwataka kuendesha shuguli hizo kwa faida ya umma.

No comments:

Post a Comment