![]() |
Bi. Nkosazana Dlamini-Zuma |
UMOJA wa
Afrika AU umesisitiza juu ya kuweko udharura wa kuchukuliwa hatua za pamoja za
kukabiliana na kundi la kigaidi la Boko Haram la nchini Nigeria.
Taarifa ya Umoja wa Afrika imezitaka nchi
wanachama wa umoja huo kuchukua hatua za maana na za pamoja za kupambana na
kundi la Boko Haram ambalo limehatarisha usalama wa Nigeria na nchi jirani na
nchi hiyo.
Mkutano wa Umoja
wa Afrika ulianza jana katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa ajenda kuu
zikiwa ugonjwa wa Ebola na Boko Haram. Akihutubia katika kikao cha ufunguzi wa
mkutano huo, Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika,
amezitaka nchi wanachama wa AU kuchukua hatua za pamoja za kukabiliana na tishio
la Boko Haram. Kwa upande wake Carlos Lopez Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya
Kiuchumi ya Umoja wa Mataifa Kwa Ajili ya Afrika amesema katika hotuba yake
kwenye mkutano huo kwamba, ukosefu wa amani unaotokana na ugaidi unakwamisha
uwekezaji vitega uchumi barani Afrika. Aidha Lopez ametaka nchi tatu
zilizokumbwa na Ebola za Liberia, Sierra Leone na Guinea Conakry zifutuwe
madeni.
No comments:
Post a Comment