![]() |
Wachezaji wa DRC |
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesonga mbele baada ya kumaliza ikiwa ya pili kwenye kundi B nyuma ya Tunisia ambayo nayo pia imesonga mbele ikiwa ndio inayoongoza kundi hilo.
Pamoja na kwamba imemaliza ikiwa na pointi sawa na Cape Verde idadi kubwa ya magoli iliyofungwa ndio iliyowavukisha.
Goli la pekee la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambalo ndilo lililowavukisha kusonga mbele lilifungwa na Jeremy Bokila. Na lile la Tunisia lilifungwa na Ahmed Akaichi.
No comments:
Post a Comment