Tuesday, January 27, 2015

REAL Madril yasaini mkataba na NSSF kujenga na kuendesha kituo cha michezo nchiini TANZANIA



Mkurugenzi mkuu wa NSSF DK Ramadhan Dau(kushoto) na Rayco Garcia wakisaini mkataba 
KLABU  tajiri duniani, Real Madrid ya Uhispania imesaini hati ya makubaliano na Shirika la hifadhi ya Jamii Tanzania (NSSF) kwa ajili ya kujenga na kuendesha kituo cha michezo kitakachogharimu Shilingi bilioni 16.

Ujenzi huo utajumuisha viwanja vitano vya mpira wa miguu, mabweni ya wachezaji na wageni, maduka na huduma nyingine muhimu .
Pia watajenga uwanja wa gofu wenye mashimo 18 utakaoambatana na ujenzi wa nyumba za kisasa katika eneo la ekari 400 lililopo katika mji uliopangwa kuwa wa kisasa wa Kigamboni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Makubaliano yalifanyika jijini Dar es Salaam muda mchache baada ya maafisa wa Real Madrid, akiwemo mkuu wa vituo vya kulelea wachezaji wa Real Madrid, Rayco ambaye wakati wa uchezaji wake alicheza na Ronaldo de Lima, Roberto Carlos na Zinedine Zidane. Kwa sasa ni kocha wa kikosi cha timu ya Real Madrid chini ya miaka 19.

No comments:

Post a Comment