Thursday, January 29, 2015

WATUMISHI wilayani Kilombero washajishwa ujasiriamali


Mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala (kulia)
WATUMISHI wa umma Halmashauri ya wilaya ya Kilombero wametakiwa kutumia fursa zinazowazunguka  ili kuongeza kipato.

Agizo hilo lilitolewa na mkuu wa wilaya hiyo Hassan Masala katika utaratibu wake wa kuzungumza na watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na kupeana taarifa za changamoto katika utumishi huo.

Masala alisema wilaya hiyo ina fursa nyingi ikiwemo ardhi byenye rutuba wanayoweza kuitumia kuzalishia mazao mbalimbali yakiwemo ya biashara na chakula na kujiongezea kipato badala ya kutegemea mishahara.

Mkuu huyo wa wilaya alibainisha kuwa mtumishi asiyejishughulisha katika kujiinua kiuchumi na kukimbilia kushabikia siasa hatakuwa na nia ya kulitumikia taifa kama alivyoomba kulitumikia na ajiande kuwapisha wenye nia na taifa.

Kuhusu matatizo mbalimbali yanayowatokea maeneo ya kazi,mkuu huyo aliwataka watumishi hao kuwasiliana moja kwa moja naye ama mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo badala ya kukaa na madukuduku yanayopedaiwa kudharau juhudi za serikali.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Azimina Mbilinyi aliwataka watumishi hao kufuata maadili  ya utumishi wa umma hasa katika mavazi kwa kuvaa mavazi ya heshima na sio mavazi ya kihuni ambayo upelekea mtumishi kudharauliwa na jamii anayoishi nayo na pia kuacha ulevi uliopindukia.

Azimina alisema kuwa mtumishi yeyote wa umma atakayemuona akivaa yeboyebo kazini atazuia mshahara wake kwani atakuwa ameonyesha picha mbaya  kwa jamii aliyokuwa nayo karibu na kusema kuwa suala la usafi ujenga heshima ya mtumishi wa umma kwa jamii.

No comments:

Post a Comment