Thursday, January 29, 2015

SERIKALI yakumbushwa kuwajali wakulima kupitia katiba pendekezwa


Mkulima wa muwa akiwa shambani
SERIKALI imeshauriwa kutathmini kwa kina mapendekezo ya katiba pendekezwa hasa katika kipengele cha wakulima kwa kuweza kuwatafutia masoko ya mazao. 

Ushauri huo umetolewa na aliyekuwa mwenyekiti Chama cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Dar es Salaam John Guninita katika mazungumzo na mwandishi wa habari hizi mjini Ifakara akifafanua zaidi alisema mbali na kukamilika kwa katiba hiyo bado sera za mazao mbalimbali ziboreshwe kwa lemgo la kukuza masoko.

Guninita alisema serikali katika kumthamini mkulima inabidi ichukue hatua za makusudi katika kukabiliana na masoko binafsi kwa kuandaa utaratibu wa kutenga ruzuku ili mazao ya wakulima yasishuke bei kiholela kuinua uchumi wa mkulima.


Amebainisha kuwa hakuna sababu ya wakulima kukosa masoko na kutolipwa pensheni tokana na kazi yake nzuri anayofanya kwani hivi sasa wanaelewa kwa kina sera ya uzalisha kwa kuweza kuwatumia wataalamu,pembejeo na kufahamu umiliki wa ardhi ili mashamba yao yaweze kuwezeshwa.

Kuhusu serikali kutenga ruzuku kwa ajili ya mkulima,Guninita alisema njia hiyo itamsaidia mkulima kutoshuka zao mazao yao bei kwani pale inapotokea serikali kwa kutumia ruzuku itaweza kusaidia kwamba bei inaendelea kusimama palepale.

“Sisi wakulima tuna matatizo makubwa tofauti na wenzetu wafugaji kwani maeneo mengi hasa kama huku vijijini kilo moja ya mchele ni shilingi 1000 lakini wenzetu wafugaji wanauza kilo moja ya nyama kwa shilingi 7000 na hapo unaona kabisa hakuna ulinganifu kati ya mkulima na mfugaji,

No comments:

Post a Comment