Thursday, January 29, 2015

MTOTO wa miaka nane ahojiwa na Polisi



MTOTO  mwenye umri wa miaka 8 ahojiwa na polisi nchiniUfaransa kwa nusu saa Jumatano baada ya madai kwamba alitoa matamshi ya kuwasifu magaidi akiwa shuleni.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la AP, mtoto huyo alikataa kuungana na wenzake darasani kwa kimya cha dakika moja kuwakumbuka watu 12 waliouawa na wanaume wawili waliokuwa wamejihami mjini Paris Ufaransa mapema mwezi huu.
Shambulizi lilitokea katika ofisi za jarida la vibonzo la Charlie Hebdo Januari tarehe saba kufuatia hatua ya jarida hilo kuchapisha picha za kumkejeli mtume Mohammad wa dini ya kiisilamu.
Wahariri wakuu wa jarida hilo pamoja na wafanyakazi wenginge waliuawa.
Mwalimu wa mtoto huyo alisema kuwa hakukataa tu kuungana na wenzake kwa kimya cha dakika moja bali pia aliwasifu washambuluaji.
Na kwa sababu ya hali ya usalama ilivyo nchini Ufaransa kwa sasa, mwalimu mkuu aliamua kumripoti mtoto huyo kwa polisi. Hata hivyo afisaa mmoja alisisitiza kwamba hakuna malalamiko yaliwasilishwa dhidi ya mtoto huyo.

No comments:

Post a Comment