Tuesday, February 10, 2015

BBC yatahadharisha kuhusu matapeli



IDHAA ya Kiswahili ya BBC inataka kuwatahadharisha wasikilizaji na watumiaji wa mtandao wake dhidi ya watu wenye nia mbaya wanaotumia jina la BBC kwa vitendo vya kitapeli.

Kumezuka mtandao bandia unaotumia jina la BBC SWAHILI NEWS kuandika habari za uzushi na kulaghai wananchi kwa habari zisizokuwa na ukweli wala uhusiano na shirika hili la habari.
BBC inapenda kuwakumbusha wasikilizaji na wasomaje wake wote wanaofuatilia habari zake kuwa makini na haina blog ya aina hiyo.

No comments:

Post a Comment