MBIU ya Maendeleo Media Group kuendesha kipindi cha Dira ya Mazingira katika redio jamii wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro.
Mhariri mkuu wa Mbiu ya Maendeleo Media Group na Msimamizi mkuu wa kipindi cha Dira ya Mazingira Bi Salma Mlamila ameeeleza hayo mwishoni mwa juma wakati akiongea na wadau wa mazingira wilayani Kilosa kwa njia ya simu.
Kipindi hicho kitaanza kurushwa rasmi februari 16, mwaka huu katika kituo cha Radio Jamiii kinachomilikiwa na Halmashauri ya wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.
Kwa takribani wiki mbili kipindi hicho kitagusa sekta ya Misitu na kitakuwa kikizungumzia jitihada za wakala wa Huduma za misitu nchini(TFS)katika kutunza, kusimamia na kuhifadhi misitu na siku ya jumatatu kitakuwa kikimuhoji Meneja wakla wa misitu wilaya ya Kilosa Bwana John Olomi.
No comments:
Post a Comment