Monday, February 16, 2015

VIONGOZI wa Afrika waanza mkutano Jijini Yaounde,nchini Cameroon



Viongozi wa Afrika wakiwa katika Mkutano

VIONGOZI  wa nchi sita wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya  Katikati mwa Afrika (ECCAS) wameanza mkutano wao wa siku mbili katika mji mkuu wa Cameroon, Yaoundé, kujadili mbinu na mikakati itakayoumiwa kukabiliana na kundi la kigaidi  la Boko Haram nchini Nigeria.

Marais Paul Biya (Cameroon), Idris Deby (Chad), Ali Bongo (Gabon), Dennis Saso Nguesso (Congo), Teodoro Obiang (Equatorial Guinea) na Catherine Samba Panza (Jamhuri ya Afrika ya Kati) wanahudhuria mkutano huo ambao pia unahudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Angola.
Nigeria haijawakilishwa kwenye mkutano huo licha ya kuwa, kundi la Boko Haram linalojadiliwa hapo linatoka katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Wiki iliyopita pia, kulifanyika mkutano mwingine wa viongozi wa baadhi ya nchi za Kiafrika ambao walikubaliana kuunda kikosi chenye nguvu cha kieneo kitakachokuwa na wanajeshi 8700 kwa ajili ya kukabiliana na kundi la kigaidi la Boko Haram.
Kundi hilo la kitakfiri katika siku za hivi karibuni limepanua wigo wa mashambulizi na hujuma yake hadi katika nchi zinazopakana na Nigeria za Chad, Cameroon na Nigeria.

No comments:

Post a Comment