![]() |
Sheikh Ponda akiwa mahakamani |
SHAHIDI wa nane G 1293 DC Abdalah dhidi ya kesi ya katibu wa Jumuia ya
waislamu Ponda Issa Ponda amekana kumsikia mtuhumiwa akitoa maneno yoyote ya
uchochezi dhidi ya dini nyingine.
Akito ushahidi mbele ya hakimu
mfawidhi mkazi Marry Moyo Asikari huyo wa idara ya upelelezi mkoa alisema mbali
na siku ya tukio kupewa kazi ya kurekodi mhadhara wa shehe Ponda hakusikia neno
lolote ambalo lingesababisha athari katika imani nyingine.
Alisema mbali na kazi hiyo hakuwahi
kusikia mlio wowte wa mlipuko katika eneo la tukio wala Shehe Ponda kupigwa
risasi hadi mwisho wa mhadhara huo.
“Baada ya kurekodi nilifikisha kwa
mkuu wangu kisha kurudisha nyuma kazi niliyorekodi kumwonyesha mkuu wangu wa
kazi kisha niliigunga na kumkabidhi vifaa vya kurekodia ikiwemo kamera”alisema G1293
wakati akihojiwa na wakili wa utetezi Juma Nasoro akisaidiwa na Abubakar Salim.
Hata hivyo akiongozwa na wakili wa
mashitaka Bernard Kongola akisaidiana na George Balasa shahidi huyo
aliithibitishia mahakama kuwa kilichorekodiwa kwenye kamera hiyo ni sahihi na
kuitaka mahakama kukiamini kwakua kamera haiwezi kupoteza kumbukumbu kama
ilivyo kwa mwanadamu.
“kilichorekodiwa ni sahihi kwakua
hiki ni chombo ambacho hakiwezi kupoteza kumbukumbu tofauti na binadamu ambae
anaweza kusaweza kusahau au kuchanganya taarifa”alifafanua shahidi G1293 na
kukabidhi kama kielelezo mahakamani hapo.
Baada ya shahidi kukamilisha
ushahidi wake,wakili wa mashitaka Bernard Kongola aliiomba mahakama kuahilishwa
shauri hilo hadi Februari 26 watakapomleta shahidi wa tisa na wa mwisho kati ya
15 waliotaraji kuwaleta dhiidi ya shitaka hilo ombi lililokubaliwa na pande
zote na kesi kuahilishwa.
Baada ya kuahilishwa kwa mahakama
hiyo wakili wa utetezi Juma Nasoro aliwaambia waandishi kuwa uamuzi wa
mashitaka kupunguza mashahidi ni ishara njema kwa mteja wao kuendelea kutaabika
na unawaonyesha upande wa mashitaka hawana ushahidi wa kuntia hatiani mteja
wao.
“kwa mujibu wa sheria hatua
inayofuata baada ya washitaki kufunga ushahidi tutakwenda katika hatua ya pili
kuona kama mshitakiwa anakesi ya kujibu au laa…kwa upande wetu mpaka sasa
hatuoni ambapo Ponda anabanwa na sheria kama alivyoshitakiwa”alisema Nasoro
Alisema kwa mujibu washitaka nikuwa
mteja wao anashitakiwa kwa kutoa maneno ya kuumiza hisia ya dini nyingine na
pili kuhamamsisha waislamu kufanya mkutano usio halali ambapo mpaka sasa hakuna
shahidi hata mmoja aliyeshuhudia Ponda kutoa ushahidi huo.
“kwa mtazamo wetu mpaka sasa Ponda
hana kosa maana hakuna aliyethibitisha kuumizwa kwa dini nyingine badala yake
mashahidi wanachanganyana wakisema waislamu mara wakristo wengine wapani na
hakuna pia aliethibitisha Ponda kushawishi mkutano usio halali…wameleta ‘clip’
ya video hapa nayo hakuna sehemu Ponda akisikika kutamka maneno kulingana na
kosa lilivyo”alifafanua
Hakimu mfawidhi mkazi Marry Moyo
aliahilisha shauri hilo hadi Februari 26 mwaka huu ambapo upande wa mashitaka
unataraji kufunga ushahidi wake kwa kumleta shahidi wake wa Tisa na kumpatia
nafasi hakimu kutafsiri sheria endapo shehe Ponda anakosa la kujibu au laa.
No comments:
Post a Comment