Tuesday, February 10, 2015

MBUNGE Abood atakiwa kujibu tuhuma za ufujwaji wa fedha


Mbunge wa Morogoro mjini ccm Abdulaziiz Abood
MBUNGE wa jimbo la Morogoro mjini Abdalahazizi Abood na Diwani kata ya Kichangani John Waziri juzi walidaiwa  kufuja fedha za shule hiyo shilingi Mil.1.5 kisha kuikosesha vyoo vya kujisaidia wanafunzi.


Abood alifika kwa dharula na kuondoka haraka shuleni hapo baada ya wazazi kumtaka kufika hapo kujibu tuhuma mbalimbali zinazo mkabili dhiidi yao ikiwemo ya kumzuia Deograthias Mbeleselo asijenge matundu sita ya vyoo kwa dharula,kauli chafu dhiidi ya mzazi huyo kuwa vyoo hivyo akajenge uwanjani Nanenane kwa ajili ya maonyesho na ukwapuaji fedha za shule hiyo.

Kwa mujibu wa wazazi hao Mbunge huyo,diwani na afisa mtendaji kata hiyo aliyetajwa Ashura Ramadhani wamewafanya kitega uchumi kwa muda mrefu kuawachangisha fedha ambazo mwisho wasiku hazijulikani zilipo na kuwa msaada wa Mbeleselo kujenga matundu hayo ulikuwa wa msaada kwao kutokana na kutokuwa na uwezo kumudu ujenzi huo haraka.

Wakizungumzia sakata hilo mzazi Mbeleselo,Makamu mwenyekiti wa kamati ya shule Akwa Liko na Mwalimu mkuu wa shule hiyo Anna Masawe mbali na kukili shule kutokuwa na vyoo kwa muda mrefu walisema changamoto inayoitafuna shule hiyo ni itikadi za vyama hasa sasa hivi kuelekea uchaguzi mkuu.

“yaani sakata hili lilianza miezi kadhaa iliyopita,mimi nimejitolea kujaga vyumba vitatu vya madarasa kwa kwa tofari za blok kwa shilingi Mil.9 ukilinganisha na shilingi Mil.18.8 walizotumia kuinulia vyumba vya aina hiyo sekondari ya kata Kola hill…tatizo niliwania uenyekiti mtaa wa Kwamchuma kupitia Chadema”alisema Mbeleselo.


No comments:

Post a Comment