Tuesday, February 10, 2015
WALIMU kuandamana mwezi April 2015 kutokana na kutolipwa deni lao
MGOMO mkubwa wa walimu mjini Kigoma unanukia mwishoni mwa mwezi Aprili kufuatia maagizo ya baraza kuu la chama cha walimu lililokutana 23/1/2015 mjini Morogoro endapo seriakali itaendelea kukaidi kutekeleza pamoja na maazimio mengine kutolipa deni lao lianalozidi shilingi Mil.342.
Kwa mujibu wa katibu wa CWT Manspaa ya Ujiji Kigoma Adam Bayinga uamuazi huo ni unakwenda sambamba na azima ya utekelezwaji maazimio ya baraza la chama hicho Taifa,na kurejesha ari ya kada ya ualimu kulitumikia taifa kwa moyo mmoja wa kuliendeleza taifa.
“katika maazimio ya baraza lile kulikuwa na agizo kwa seriakli utekelezwaji wa makubaliano wa nyaraka mbalimbali ikiwemo azimio la walaka wa utumishi namaba 1 wa 2014 kumbu na AC.87/260/01/G/9.15/7 wa 2014 juu ya muundo wa utumishi kada ya ualimu chini ya WEMU”alisema Bayinga.
Katika ufafanuzi wake alisema katika waraka huo ulioanza 1,Julai,2014 muundo wa utumishi kada ya ualimu umebadirika na kuongezwa mishara na madaraja ya utumishi kwa ongezeko la madaraja mawili kwa mwalimu wa daraja III A,stashahada na shahada ongezeko la daraja moja kila kiwango cha elimu.
Alisema chama hicho Kigoma kinaunga mkono kuwa watakuwa tayari kufanya hivyo ifikapo 30 Aprili kutokana na walimu hao kuteseka bila msaada wowote dhiidi ya changamoto wanazokutananzo ikiwemo kutopanda au kupanda madaraja bila maboresho ya stahiki zao,kutolipwa madaia yao likiwemo la likizo,uhamisho,matibabu na mengineo.
Katibu huyo aliongeza deni la zaidi ya shilingi Mil.342 ni la hadi Desemba mwaka jana ambapo seriakali imelifumbia macho ikiwapuuzaa walimu na kuongeza kuwa suala la mabadiriko ya muundo wa mifuko ya hifadhi ya jamii kupitia Mamalaka ya mifuko hiyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment