MTU mmoja asiyefahamika jina mwenye jinsia ya kiume
anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka(35) hadi arobaini amefariki dunia
baada ya kugongwa na treni katika eneo la Kingolwira manispaa ya Morogoro.
Wakizungumza
na kituo hiki wananchi walioshuhudia tukio hilo akiwemo mwenyekiti wa
mtaa wa ujenzi Christopher Charles Chizza na wananchi Aloyce mdoe
wameelezea kuhusiana na ajali hiyo .
Hata
mwenyekiti wa mtaa huo ambao tukio hilo limetokea amesema wao wamepata
taarifa ya kutokea ajali hiyo majira ya asubuhi kupitia
kwa wananchi ambao wanatumia njia hiyo ambapo amewataka wananchi
kutofanya vitendo vya kikatili kwa binadamu na kuwatupa relini kwa visingizio
vya kugonjwa na tren.
Kwa
upande wake mkuu wa stesheni ya Reli Morogoro ya TRL Bwana
Flavian Nyawale Mukoba ameelezea kuhusiana na ajali hiyo ambapo pia
ametoa wito kwa wananchi hususan wanaotembea kwa miguu au usafiri
wa pikipiki na baiskeli kuwa waangalifu wanapotembea kwenye reli
hiyo kwa ajili ya usalama wao.
Mwili
wa marehemu huyo umechukuliwa jeshi la polisi mkoani morogoro
kwenda umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya
rufaa mkoa wa morogoro kwa ajili ya kutambuliwa na ndugu zake.
No comments:
Post a Comment