Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon |
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa ushirkiano wa watu wote duniani ili kupunguza majanga.
Ban ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kongamano la tatu la Umoja wa Mataifa kuhusu kupunguza majanga linaloendelea mjini Sendai, Japan.
Katibu Mkuu amesema mkutano huu ni dalili ya kuelekea katika mustakabali mwema na endelevu na kuongeza kuwa safari hii ya matumaini inaanzia Sendai.
Sendai mji uliko eneo la Tohoku uliathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi nchini Japan na tetemeko la baharini Tsunami mwaka 2011.
Miaka minne badaye wakuu wa nchi, mawaziri, na viongozi wengine wanakutana kwa ajili ya mikakati thabiti kwa ajili ya dunia salama.Ban amesema huu ni wakati wa kuwezesha watu na kusaidia jamii kwa rasilimali akitolea mfano kuwa tetemeko la ardhi katika nchi moja laweza kuathiri uchumi wa mataifa mengine. Inakadiriwa kuwa zaidi ya kiasi cha dola bilioni 300 kinahitajika duniani kwa ajili ya kupunguza majanga ya asili. Moja ya matokeo yanayotarajiwa kupitia kongamano hilo ni kupitishwa kwa mkakati mpya utakaookoa maisha ya watu na kupunguza gharama za uharibifu kutokana na majanga ya asili.
No comments:
Post a Comment