Jengo la CWT Morogoro |
KIVUMBI cha kupata viongozi wapya watakao kiongoza chama cha
waalimu CWT nchini kwa miaka mitano ijayo kinaanza kutimuka leo(Mach 18) kwa
chama hicho Manispaa ya Morogoro kufanya uchaguzi wake ambapo zaidi ya
wanachama 100 wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi mjini humo.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi mjini ofisini kwake,katibu wa CWT mjini humo,Raphael Maswi alisema
maadalizi yamekamika akiainisha kuwa karibu jumla ya nafasi 15 zitagombewa na
waombaji wa nafasi hizo.
"nafasi zinazogombewa na zinaonyesha
kuwa na ushindani mkubwa ngazi ya wilaya ukiacha ya katibu alieajiliwa na chama
ni pamoja na Mwenyekiti inayopwaniwa na watu nane pia Mwekahazina watu
nane" alisema Maswi.
Mbali na nafasi hizo pia nafasi
nyingine waniwa ni mwakilishi kitengo-Ke,Walemavu,vijana,Utawala, Mahitaji
maalumu,wakilishi wanne Shule za msingi,Awali,Sekondari,vyuo vya ualimu,vyuo
vya ufundi na waliomba kamati ya utendaji.
"ni mkutano mkuu utakaokuwa na
agenda moja tu ya Uchaguzi na baada ya hapo utafauatiwana uchaguzi ngazi ya
mkoa ambapo hawa watakuwa wajumbe wake"aliongeza.
Aidha alisema kwa kipindi kifupi
chama kimekuwa na mafanikio makubwa katika uendeshwaji wake jambo
lililosababisha walimu wengi kujiunga na kufikia asilimia 98 sasa
ikilinganishwa na asilimia 60 miaka mitano iliyopita.
mafanikio mengine ni kuanzishwa kwa
Benki ya walimu itakayotoa mikopo kwa mashariti nafuu na kuboresha vivutio
ikiwemo utoaji zawadi kwa wastaafu na uendelezaji walimu katika maendeleo na
elimu.
No comments:
Post a Comment