Mwalimu Rehema wa Morogoro sekondari akitoa sera katika Uchaguzi wa CWT Mkoa wa Morogoro |
KATIBU wa chama cha walimu CWT mkoani Morogoro Issa
Ngayama amekerwa na taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa walimu mkoani humo
wamegeuka changudoa na kuwataka waliovamia taaluma hiyo kwa njaa kutafuta pori
jingine badala ya kuidhalilisha.
Akizungumza kwa hasira dhidi ya taarifa hizo kwenye mkutano wa
uchaguzi wa viongozi CWT Manspaa,Ngayama aliwataka walimu mkoani humo kuanza
kuchunguzana tabia yakiwemo maadili na haiba ya ualimu.
“walimu wenzangu nimekelwa sana na hili na niwatake ninyi
mkajitafakari huko hivi umeingia kwa wito au bahati mbaya! Kama ni kwa bahati
mbaya niwatake mkatafute pori linguine sio kuvamia fani hii kwani hii inamiiko
yake!..ualimu ni taaluma na mfano katika maadili”alifafanua
Mbali na hilo alisema walimu wa sasa wamekuwa kituko kwa jamii
kutokana na kutoheshimu mifumo ya utumishi wa kada hiyo kwa walimu kuwa vinara
wa mavazi ya anjabu ajabu na kauli mbaya dhiidi ya watoto nje na madarasani.
"hivi kweli mwalimu unaingia darasani umevaa kujinzi
kimebana,nguo za kulalia,kinguo kinaonyesha viungo,makalio na kauli zako kama
mvutabangi hivi watoto watakuwa vipi...kumbukeni mnaaminiwa kuliko yoyote mbele
za
watoto na jamii sasa katika hali kama hii mnaweza kuitwa
hivyo"alisisitiza.
Katika uchaguzi huo uliohudhuliwa na Afisa utumishi na utawala cwt
Taifa Ally Kambi, Katibu huyo wa mkoa alimtangaza mratibu elimu kata ya
Chamwino Patrick Mng’ong’o alichaguliwa kwa kura 72 dhiidi ya kura 95 kuwa
mwenyekiti cwt manspaa kwa miaka Mitano ijayo.
Mbali na Patrick kuwabwaga wenzie saba pia Ngayama aliwatangaza
wengine kura kwenye mabano Novatus Mzaga(81) aliewabwaga watu saba dhiidi,
mwakilishi kitengo ‘ke’ shule ya msingi Jane shoo (46),mwakilishi ‘ke’
sekondari Elizabeth Werema kwa kura (70)
Kwa mujibu wa msimamizi huyo mwakilishi vijana walemavu
alichaguliwa Agnes Mbaga(46),Mwakilishi walimu wa vyuo Francisca
Chilongozi(48), wawakilishi wanne shule za msingi Gaston Lyuma,Hildegarda
Kimotuo,Mary Mlewa na Mloka Karoli,
Uchangudoa upo idara zote, siyo walimu pekee, lakini nguvu ya pamoja inahitajika kuondoa tatizo.Juma Salumu wa Mzumbe, Morogoro
ReplyDeleteUchangudoa ni janga la kitaifa, siku hizi kila mkoa kuna maeneo maalumya biashara ya ukahaba.Tunakwenda wapi?Lusekelo Mbangwa wa Iringa
ReplyDelete