Friday, March 20, 2015

MBUNGE alalamikia tatizo la maji mkoani Tanga



Wabunge wakiendelea na kikao Bungeni mjini Dodoma
MBUNGE wa Lushoto (CCM), Henry Shekifu, amelalamikia tatizo la maji mkoa wa Tanga na kuilaumu serikali kwa kutoa ahadi za mara kwa mara huku ikishindwa kuzitekeleza.



Akiuliza swali bungeni mjini Dodoma jana, Shekifu alisema kwa muda mrefu serikali iliahidi kupeleka maji katika wilaya ya Muheza lakini haijatimiza.
Aidha, Shekifu alitaka kuhakikishiwa kama kuna fungu lolote lililotengwa kwa ajili ya utekelezaji miradi ya maji katika wilaya hiyo kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha.
“Serikali inatamka nini katika ahadi zake ambazo hazionyeshi kutekelezwa,” alihoji.
Katika swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Al-Shaymaa Kwegyir, lililoulizwa kwa niaba yake na Shekifu, alitaka kujua ni kwa nini hadi sasa hakuna juhudi za makusudi za kuhakikisha maji yanapatikana kutoka Mto Zigi ili kumaliza tatizo sugu la maji mkoani Tanga, hususan Muheza.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maji, Amosi Makalla, aliwaomba wabunge kuunga mkono bajeti ya wizara hiyo pale muda utakapofika ili fedha za kutosha zitengwe kwenye miradi mbalimbali mkoani Tanga.
Alisema miradi yote iliyo kwenye ahadi ya serikali itafanyiwa kazi na kukamilishwa kulingana na uwezo wa kifedha utakavyoruhusu.
Kwa mujibu wa Makalla, ili kutatua tatizo la maji katika mji wa Muheza, serikali imeandaa mpango wa muda mrefu wa kuboresha huduma hiyo kwa kutoa maji kutoka Mto Zigi hadi Muheza mjini na vitongoji vyake.












4 comments:

  1. Hii ni wiki ya maji lakini kuna mikoa maji hayapatikana.Hongera Mbunge Shekifu kwa kuliona hilo.

    ReplyDelete
  2. Maji safi ana salama yanapatikana ?Huku Mbezi Dar, maji kweli ni shida.Serikali ituangalie.Ni mama Kauthari

    ReplyDelete
  3. Mpwapwa maji si salama chumvi imezidi sana .Wiki ya maji iangalie namna ya kutupatia wananchi wa Mpwapwa na vijiji vyake maji safi na salama.

    ReplyDelete
  4. Kilombero maji ni mengi, lakini usalama usafi na usalama ndio tatzo.Maiko wa Ifakara.

    ReplyDelete