Friday, March 13, 2015

IDARA ya Maliasili wilaya Kilosa kuzungumza katika kipindi cha Mazingira



IDARA ya maliasilia wilaya ya Kilosa itakuwa ikielezea mikakati na kazi mbalimbali inazozifanya katika Halmashauri ya wilaya ya Kilosa , mkoa wa Morogoro kwenye  kipindi cha Dira ya  Mazingira kupitia Redio Jamii iliyopo Kilosa.

Akiongea na Muandaaji wa kipindi cha Dira ya Mazingira, Mkuu wa Idara ya Maliasili wilayani humo, Bwana Ibrahimu Ndembo amesema kuwa wasikilizaji wajiandae vyema kupata mengi kuhusu kazi na majukumu ya Idara hiyo.

Mzungumzaji katika kipindi cha kesho atakuwa Bwana Abdallah  Mazingira ,mmoja wa wataalamu katika  Idara hiyo.

4 comments:

  1. Hao ndio muhimu sana tunawahitaji,maana wananchi hawatambui mchango wa maliasili katika maendeleo

    ReplyDelete
  2. Huyo mzungumzaji anafanana na kipindi .sasa tunasubiri atueleze maliasili za nchi zinatumikaje na wao wanawasaidia vipi wananchi wa vijijini

    ReplyDelete
  3. Tunaomba turuhusiwe maswali katika kipindi cha kesho

    ReplyDelete
  4. TUNAKISUBIRI KWA HAMU KIPINDI CHA KESHO CHA MALIASILI.OMMY WA UHINDINI KILOSA

    ReplyDelete