![]() |
Kamanda wa polisi Kaunti ya Mombasa Robert Kitur |
INSPEKTA
wa Polisi Ibrahim Mohammed ameuawa kwa
kufyatuliwa risasi na watu wenye silaha huko Mombasa, nchini Kenya.
Jeshi la Polisi la Kenya limeeleza kuwa,
watu hao waliobeba silaha hawakumjeruhi mtu yeyote baada ya kutekeleza
shambulio hilo.
Robert Kitur Kamanda wa Polisi Kaunti ya
Mombasa amesema kuwa, bila shaka shambulio la kumuua Inspekta Ibrahim Mohammed
lilipangwa na makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka nchini humo. Hayo
yanajiri katika hali ambayo, tokea serikali ya Kenya ilipoamua kupeleka majeshi
yake nchini Somalia kwa shabaha ya kukabiliana na kundi la al Shabab, nchi hiyo
imekuwa ikikabiliwa na mashambulio ya mara kwa mara ya kigaidi na hasa katika
Kaunti za Wajir, Mandera na Mombasa.
No comments:
Post a Comment