![]() |
Mkulima wa ndizi kijiji cha Ulaya, wilayani kilosa |
WAKULIMA
wa zao la ndizi katika vijiji vya Kidodi na
Ulaya wilayani Kilosa, mkoani Morogoro, wameiomba serikali wilayani humo
kuwasaidia katika kuwatafutia masokoya uhakika ya zao hilo.
Wakiongea na kipindi cha Dira ya
Mazingira katika vijiji hivyo, wakulima hao wamesema kuwa, bado wakulima wa zao
la ndizi hawana uhakika wa kutosha kuhusu soko la ndizi,kwani wanapata tabu
sana kuuza mazao kipindi cha uvunaji.
Wamesema ukosefu wa soko la uhakika
ndani ya wilaya kumesababisha zao hilo liuzwe kwa bei ya chini , ambapo mkungu
mmoja uuzwa kati ya shilingi elfu tatu na elfu nne.bei ambayo haiendani na
gharama za uzalishaji.
No comments:
Post a Comment