Monday, March 23, 2015

WAKULIMA wamuomba mkuu wa mkoa kuwarejeshea shamab lao


Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk. Rajabu Rutengwe
USHIRIKA wa wakulima na wafugaji ‘Twende Pamoja’ wilayani Morogoro,Manispaa na Mvomero mkoani Morogoro umemuomba mkuu wa mkoa huo Dk.Rajabu Rutengwe kuwarejeshea shamba lao kijijini Mela-Mvomero baada ya kupokwa na kutiwa hasara ya zaidi ya shilingi Bil.1.65.


Shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 1,500 linadaiwa kupokwa na viongozi mbali mbali wa serikali akiwemo aliyekuwa mkuu wa mkoa Said Kalembo na wakuu wa wilaya Samweli Kamote na Hawa Ng'humbi ambao sasa hawapo madarakani.

Mbele ya mkuu wa wilaya ya Mvomero Festo Kiswaga kwa niaba Dk Rutengwe mwishoni mwa wiki,mwenyekiti wa ushirika huo Ally Hawaya na risala ya washirika iliyosomwa na Mwajabu Haji walimwambia mkuu huyo kuwa hasara hiyo ilitokana na uwekezaji kwenye eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 1500.

 “ushirika huu upo kisheria tangu 19/11/1999 kwa usajili MRG 245 na wanachama 1,442 tukilenga kuwakwamua watu hususani vijana na umasikini kupitia kilimo na ufugaji…tayari tulishaanza kuwekeza kwa kufyeka misitu na kulima,kuchimba bwawa la umwagiliaji na mifugo pia topografi kwa ndege”alisema Hawaya.

Alisema ushika huo mbali na kuwekeza kiasi hicho kilicho shwishi na kuvutia vijana wengi kushiriki katika sekta hizo za uzalishaji serikali kupitia wakuu wa wilaya watano na mkoa wawili walibadili azima hiyo na kuwanyang’anya ardhi kasha kuwapa wafugaji jamii ya Masai ambao walijeruhi wakulima na mauaji.

“Katika risala yao pamoja na mambo mengine Mwajabu alinukuu baadhi ya barua zilizopuuzwa kuwa ni pamoja naya 25/8/2003 kumbu MVD.60/277 kwa katibu CCM mkoa na barua ya 30/11/2007 kumbu MVD/D.30/18/83 kwa mkuu wa wilaya.

Kuhusu uthibitisho wa uhalali wao katika umilikaji eneo hilo Mwajabu alinukuu barua ya mkurugenzi wa halamashauri ya 24/11/1998 kumbu MJD/174/27/ARM na barua ya 27/7/1999 kumbu MDC.O.40/2/VOL.11/152 na mihutasari ya kijiji ukiwemo wa 20/05/1999 na muhutasari wa 22/6/1999.

 Akijibu madai hayo Kiswaga aliushuri ushirika huo kuimarisha kiuongozi na kuhakikisha wanapata hati za umilikaji maeneo ili ziwasaidie kufanya shuguli zao za ushirika kwa uhuru na upana mkubwa wa maendeleo.

“hapa mimi kwa kiasi kikubwa ni mshauri,na ushauriwangu kwenu ni kwanza muwe na uongozi imara na hakikisheni kama ushirika ni wa kuwekeza kwenye ardhi hakikisheni mnapata hati za umilikaji ardhi ili mfanye shuguli zenu kwa uhuru na upana mkubwa”alishauri Kiswaga.

Aidha aliwashuri kutafuta maeneo mengine ya ardhi yasiyo na mgogo mkoani humo kasha kuyaombea hati miliki kabla hawajagawana huku akiahidi kuwasaidia kupata maeneo hayo endapo watahitaji msaada wake na kutoa elimu ya uendeshaji ushirika kama huo ili uwe na faida kwao

No comments:

Post a Comment