![]() |
.Mbunge wa Morogoro mjini Abdul Aziz Abood |
MBUNGE wa Manispaa ya Morogoro Abdul Aziz Abood ametoa shilingi
Mil.1.750 zitakazotolewa kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu kati ya timu 22
zinazoshiriki kombe la Ndulu Group of Companies Ltd lililoanza jana.
Abood aliahidi kiasi hicho cha
zawadi kabla hajazindua michuano hiyo na kugawa vifaa vya michezo na kufafanua
kuwa mshindi wa kwanza mbali na seti tatu ya jezi,kombe na mpira atatwa
shilingi Mil.1.
“kwa mshindi wa pili mbali na seti
mbili za jezi na mpira walizoandaliwa na mkurugenzi Castor Ndulu mimi
nawaongezea shilingi 500,000 na mshindi wa tatu mbali na pea moja ya jezi basi
namwongezea shilingi 250,000”alisema Abood.
Aidha aliwataka vijana kutojisahau
na michezo akiwahimiza kujiandikisha katika daftari la wapigakura ili washiriki
kupata viongozi wapya katika chaguzi zijazo.
Awali akimkaribisha kuzindua michezo
hiyo Mkurugenzi wa kampuni hiyo Castor Ndulu alimweleza mbunge huyo kuwa kuwa
dhamira ya michezo hiyo si kwa madhumuni ya kisiasa badalatake ni maanadalizi
ya kuandaa klabu ya soka ya Ndulu itakayokuwa mbadala wa timu zilizo ligi kuu
nchini.
“nikutahadhalishe kuwa kunabaadhi ya
wanasiasa wenzio hawakutakii mema kwa vikwazo tulivyokutana navyo wakati wa
kuomba kibali kwani wanadhani unataka kututumia sisi kisiasa…lakini niualifu
umma kuwa mashindono haya ni ya Ndulu na si vinginevyo”alifafanua Ndulu.
Hata hivyo katibu wa soka masipaa
Khafale Maharagande aliwathibitishia wanamichezo na mbunge kuwa ligi hiyo ipo
kisheria baada ya waombaji kukidhi vigezo vya uandaaji mashindano kama hayo.
Alizitaja timu zitakazo minyana
katika uwanja wa Ndetembya-Kihonda kuwa ni
Lamasia,Mgudeni,Eagle,Juhudi,Mlunda,Top Site,Lukobe B,Majengo,Jakalanda,Lukobe
A,Muungano,Uwanja wa Taifa,Tushikamane,Uwanja waTaifa,Manyuki,Blak stone,Maduka
10,Digidigi,Ndetembia,Kilongo,Palupalu na Maendeleo.
No comments:
Post a Comment