VIKUNDI
vya ufugaji wa Nyuki wilayani Kilosa
vimetakiwa kufuata taratibu na maelekezo yanayotolewa na wataalamu ili kuondokana na Umaskini wa kipato.
Ushauri huo umetolewa hivi karibuni
na Afisa Misitu na Nyuki wa Halmashauri
ya wilaya ya Kilosa Bwana Sebastian Malisa katika mahojiano na kipindi cha Dira
ya Mazingira , Radio Jamii ya mjini Kilosa .
Bwana Malisa amefafanua kuwa
wanavikundi wngi wa ufugaji wa nyuki wilayani humo wamekuwa nakawaida ya
kutozingatia kanuni na taratibu za kitaalamu kuhusu ufugaji wa nyuki hali inayochangia kuvuna asali chini ya viwango.
No comments:
Post a Comment