Mbunge wa Morogoro mjini Abdul ziz Abood |
WANAWAKE Manispaa ya Morogoro kupitia zaidi ya vikundi 148 vya silc
na vikoba mjini humo mwezi Mei wanakusudia kumpongeza mbunge wa jimbo hilo
Abdulazizi Abood kwa mchango wake wa kuwapunguzia umasikini akinamama na vijana
kwa kuvihamasisha vikundi,kuviwezesha na kuvisimamia.
Tafrija hiyo inayotaraji kufanyika
katika uwanja wa Jamuhuri mjini humo,inatarajiwa pia kumwomba atetea nafasi
yake hiyo kwa kumkabidhi fedha za fomu,kufanyika maonyesho ya bidhaa zao na
kugonganisha bunifu walizonazo kwenye vikundi ili kukuza vipato vyao.
Wakizungumzia hilo kwa nyakati
tofauti kwenye tafrija za kugawana mapato na taarifa zamwaka mwishoni mwa wiki
Mwalimu Mkuu msimamizi wa vikundi vya SILC Manspaa hiyo kupitia mradi wa
TUNAJALI Leonce Mvungu na mkufunzi kutoka CARE(T) Francis Mbwambo walisema
kupitia vikundi hivyo wananwake na vijana wamekuza vipato vya familia na jamii.
“tunaomba tufahamike kuwa tafrija
hii ni mpango wa wanavikundi baada ya kuona faida ya vikundi,lakini tunataka
kumpongeza Abood kwa umahili aliokuwa nao licha ya kutoa chochote lakini ushuri
na maagizo yake yameviwezesha vikundi kuimarika…leo tunaongelea kukua mitaji
yaani kikundi chenye mtaji mdogo kinakaribu shilingi Mil.35”alisema Mvungu.
Awali katika risala za vikundi zilizosomwa
kwa nyakati tofauti kikundi cha ‘Silc Chamwino’ na kikundi cha Umoja ni
nguvu(Kija -umongu) pamoja na mambo mengine walimwomba mbunge huyo kutovunjika
moyo wa kuendelea kuvijenga kwa kuvitafutia masoko ya bdhaa wanazobuni na
kuziandaa kukuza mitaji yao.
“mfano katika kipindi cha mwaka
2015-2016 Kija-Umongu inakusudia kukuza mtaji wake hadi zaidi ya shilingi
Mil.150 sambamba na kutafuta vyanzo vingi vya kukuza mtaji…tutapenda kupata
uzoefu wako wa hali na mali kufikia azima hiyo”alisoma Stela Mwanilwa wa
kikundi cha Kija-umongu.
Katika hotuba iliyotolewa na katibu
wake Moris Masala,Abood alivitaka vikumdi kujiimarisha kwa ubunifu mkubwa
katika kuandaa bidhaa,kuboresha ufungashaji bidhaa hizo na kuwa na nidhamu
kwenye matumizi ya fedha kwa kusoma mbele ya wnachama wote taarifa za mapato na
matumizi na kipindi wanapogawana gawio.
“unajua sasa hivi takwimu
zinaonyesha wanawake wanaweza hata wasipowezeshwa hata kwa mifano midogo
sasa hivi ndio watafutaji,waleaji familia na ndio wanaopanga familia
iishi vipi…na ninawasini akina baba muda mfupi ujao tutakuwa ombaomba kwa
wanawake zetu maana tumebaki watu wa kumka na kukimbilia vijiweni kubishana
tu”alisema Masala.
Aliwataka kuendelea kuhamasisha
wenanwake na vijana kujiunga katika vikundi hivyo ili wajiongezee ujizi wa
kutunza na kuongeza fedha katika mamilia zao.
No comments:
Post a Comment