Jengo la CWT la mkoa wa Morogoro |
WALIMU
wilayani Chemba mkoani Dodoma wamesusa posho ya shilingi 5,000 badala ya
shilingi 25,000 waliyopaswa kulipwa na idara ya Afya baada ya kuendesha zoezi
la chanjo ya kichocho na minyoo kwa watoto mashuleni.
Wanaotajwa kuendesha zoezi hilo la dhuluma
ya posho kwa walimu hao
baada ya zoezi hilo lililofanyika kati ya
Aprili 8-10 ni pamoja na Mkurugenzi wa halamashuri William Mafwele,mkuu wa
idara ya Afya wilaya DMO Dk.Sylivester Makondo na mkuu wa idara ya elimu DEO
Abdalah Mbaruku.
Wakizungumza kwa shariti la kutotajwa
majina yao kwa hofu ya kupoteza ajira zao kutokana na vitisho vinavyotolewa na
viongozi hao wakiongozwa na Mkurugenzi kwa nyakati tofauti walisema
wanasamehe fedha hizo kwa kuchoshwa na dhuruma wanazofanyiwa kila mwaka.
William Mafwele alipotafutwa kutoa
ufafanuzi wa dhuruma huyo hakutaka kutoa ushirikiano kwa mwandishi baada ya
kumtaka kuandika alichoelezwa kwakua hana muda wa kujadili upuuzi kama huo.
Hata hivyo alipotafutwa DMO Dk. Sylivester
Mkondo na DEO Abdalah Mbaruku kwa nyakati tofauti walikiri kuwepo kwa tukio
hilo wakidai kutokana na walimu kutoelewana na mratibu wa mradi huo wakati wa
semina ya utoaji chanjo hizo.
Walisema baada ya walimu hao
kueleimishwa tofauti ya malipo ya mwakajana inatokana na zoezi lile kujumuisha
mazoezi mawili likiwemo Surua na Lubela tofauti na mwaka huu ambapo zoezi
litahusu zoezi moja,walikubali na zoezi la kuwalipa shilingi 15,000 limeanza.
Kwa mujibu wa walimua hao kuchoshwa na dhruma hiyo kunatokana na
zoezi kama hilo mwakajana kudhumika badala ya kulipwa shilingi 30,000
walizostahili kwasiku badala yake wakalipwa shilingi 25,000 huku wakitishwa
kufukuzwa kazi waliojaribu kuhoji.
No comments:
Post a Comment