Thursday, April 30, 2015

WAVUVI wilayani Kilombero waomba kupatiwa elimu ya mazingira


Wavuvi katika kivuko cha mto Kilombero wakiendelea na shughuli zao
WAVUVI wanafaonya shughuli za uvuvi katika kivuko cha Mto Kilombero, Ifakara , wilayani Kilombero, mkoa wa Morogoro wameiomba Idara ya maliasili na mazingira wilayani humo kuwapatia elimu ya utunzaji wa mazingira ili kupunguza kasi ya uharibifu wa mazingira
                                                                                             

Wakiongea na kipindi cha Dira ya mazingira katika eneo hilola kivuko wiki hi, baadhi ya Wavuvi wamesema kuwa, hali ni mbaya kwa upande wa utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika eneo hilo kwani watu wengi na baadhi ya  wavuvi hawana elimu ya namna ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Wamesema , pamoja wilaya ya Kilombero kuwa na Taasisi kadhaa za mazingira hasa katika bonde la mto Kilombero ,lakini utoaji wa elimu kwa umma juu ya namna ya  utunzaji wa mazingira hauendani na uhitaji.

Wamesema kwa upande wa wananchi ambao wao ni wasafiri wamekuwa wakitenda vitendo vinavyoharibu mazingira yam to huo kwani hakuna uhamasishaji wa kutosha toka Idara husika ya mazingira sanjari na wadau mbalimbali wa mazingira ndani na nje ya wilaya.














No comments:

Post a Comment